{"product_id":"9789966181886","title":"Hazina ya Ushairi","description":"Hazina ya Ushairi ni kazi ambayo inadhamiria kuondoa ugumu wa uchambuzi wa mashairi na kuufanya uwe somo linalowezekana kusomwa,\u003cbr\u003ekufurahiwa na kuchambuliwa na mwanafunzi pasipo kumhitaji sana mwalimu wake. Ukiwadadisi wanafunzi maoni yao kuhusu somo la ushairi utagundua kuwa asilimia kubwa sana wasingalipenda litahiniwe.Kisa na maana ni kwamba linachukuliwa kuwa somo la kuogofya na walimu wengi,\u003cbr\u003efalaula mwanafunzi aliyezongwa na masomo mengine mengi 'magumu'!\u003cbr\u003eWengi hawaoni sababu ya kusumbuliwa na mashairi hasa ikikumbukwa kwamba ujuzi wake hauhitajiki mtu anaposaka gange. Mwelekeo huu hasi ni tisho kubwa linaloelekea kuangamiza fahari na umuhimu wa ushairi miongoni mwa vizazi vichanga.\u003cbr\u003eWataalamu wa awali walitunga diwani na wenzao kuzichambua.Wengi wa hao waliozichambua walisahau kutoa ushairi mikononi mwa Mswahili.\u003cbr\u003eWaliishia kuutwaa vile ulivyokuwa katika enzi za Muyaka bin Haji na kumkabidhi mwanafunzi asiyehusiana naye kwa lolote wala chochote kisha wakamtaka aipende na kuionea fahari fasihi ya Kiswahili kama alivyopenda\u003cbr\u003eMwalimu Simtaji na wengineo. Matokeo yake ni kwamba taabu za mwanafunzi hazikufikiriwa katika diwani zile wala katika tahakiki zao.\u003cbr\u003eAidha, istilahi za ushairi, hasa zenye asili ya Kiarabu, zilimkaba koo,\u003cbr\u003emsamiati wa kishairi [lugha za kilahaja] ulimzonga pumzi, na arudhi kadha zikamtisha na kumtamausha akawa mnyonge kweli. Kwa sababu hiyo, hata kazi sahili na wa kupendeza zisizohitaji tafakuri, kama vile mashairi ya\u003cbr\u003eKwa wanafunzi wa shule za upili vii watunzi wa kileo kama Alamin Mazrui, Said Ahmed Mohamed, Fikeni\u003cbr\u003eSonkoro, David Massamba, Mugyabuso Mulokozi, Kithaka wa Mberia na wengine wengi, hazipati umaarufu unaostahiki miongoni mwa vijana.\u003cbr\u003eDiwani zilizosomwa na walimu na wanagenzi wao zilikuwa zizo hizo zinazowanyima raha wanafunzi darasani. Matokeo ni kuwa vyuo vilizaa walimu wengi wasioyapenda mashairi na vitabu visivyoeleweka viliwanyima starehe. Nao waliingia navyo madarasani; kufunza ati!\u003cbr\u003eWalipomaliza kufunza wanafunzi walitamani sana somo hilo liondolewe kabisa kwenye silibasi. Hivyo basi mimi situngi diwani, nahifadhi hazina ya ushairi; kumbukumbu ya kurejelewa na mwalimu na mwanafunzi darasani.","brand":"Ariba Book Publishers","offers":[{"title":"Default Title","offer_id":47065768427760,"sku":"9789966181886","price":13.0,"currency_code":"USD","in_stock":false}],"thumbnail_url":"\/\/cdn.shopify.com\/s\/files\/1\/0737\/7593\/9824\/files\/9789966181886_p0.jpg?v=1763695167","url":"https:\/\/shop-qa.barnesandnoble.com\/products\/9789966181886","provider":"Barnes \u0026 Noble (DEV)","version":"1.0","type":"link"}